MAZUNGUMZO YA KUJIONDOA KATIKA UMOJA WA ULAYA

 

Waziri wa masuala ya Uingereza kujitenga na Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Mjumbe mkuu wa Uingereza katika mazungumzo ya nchi hiyo kujiondoa katika umoja wa ulaya, David Davis, amejiuzulu. Davis amejiuzulu kwa sababu alitofautiana na msimamo wa serikali yake ambao baraza la mawaziri lilikubaliana nao siku chache zilizopita. Kwenye barua yake ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Theresa May, Davis amesema sera na mbinu zilizoko kwa sasa, zinaifanya Uingereza kuwa na nafasi ndogo au haitajitenga na umoja wa forodha na soko moja kuu. Kwa upande wake Bibi May, amemwambia Davis kuwa hakubaliani na anavyochukulia sera ambayo walikubaliana kuhusu na baraza la mawaziri. Tayari Bibi May amemteua Dominic Raab kuwa waziri mpya wa masuala ya Brexit.