MBINU ZINAHITAJIKA KUINUA KIWANGO CHA UFAULU KWA WANAFUNZI

 

Mkuu wa mkoa wa kusini unguja mhe hassanKhatib hassan amesema mbinu mpya zinahitajika

Kati ya wazazi na walimu ili kuinua kiwango cha Ufaulu kwa wanafunzi katika skuli za mkoa huo

Mhe khatib ametoa kauli hiyo ukumbi wa tc dunga na kitogani katika kikao cha pamoja kilichowashirkisha walimu wakuu wa skuli za msingi na sekondari, wenyeviti wa kamati za skuli pamoja na masheha wa  mkoa huo chenye lengo la kutafuta changamoto zinazopelekea kushuka kwa ufaulu.

Amesema kwa mwaka uliopita matokeo ya mitihani katika mkoa huo sio mazuri   hivyo ni vyema  wazazi na walezi  kupanga mikakati mipya itakayowezesha wanafunzi waweze kufanya vyema katika mitihani yao ya taifa kwa mwaka huu.

Nao walimu hao wamesema   mashirikiano  madogo kutoka kwa wazazi na baadhi ya wanafunzi kujishiriksha katika mambo ya starehe ni miogoni mwa mambo yanayopelekea  kushuka kwa kiwango cha ufaulu.