MBIO NZA MWENGE WA UHURU KITAIFA ZIMEANZA RASMIN

 

Mbio nza mwenge wa uhuru kitaifa zimeanza rasmini   kwa kukimbizwa katika  mikoa ya tanzania  bara   ambapo kwa zanzibar  umepokelewa katika mkoa wa kusini unguja  jumanne ya tarehe 26.

Katika wilaya ya mjini  mwenge wa uhuru unatarajiwa kupokelewa tarehe 01 july  ukitokea wilaya  ya magharibi ‘b’ katika uwanja wa amani ambapo utapokelewa na mkuu wa wilaya  ya mjini  bi marina joel thomas na viongozi  mbali mbalina  vikosi vya ulinzi na usalama.

Wakati wa ukukimbizwa katika wilaya ya mjini  mwenge wa uhuru  una tarajiwa kuzindua jumla ya miradi  tisa  ya kimandeleo  ikiwemo  mradi wa  maji safi  na salama  katika  shehia  ya  chumbuni,  uzinduzi wa  kituo cha polisi kwa bitiamrani  vikundi mbalimbali vya ujasiria mali   ikiwemo vya ukulima wa  mboga mboga.

Maeneo mengine yatayo pitiwa na kuzinduliwa na mwenge wa uhuru ni  ushirika wa   wanafunzi wa wajasiria mali katika skuli ya  bembela  ambapo katibu twala wa wilaya ya ya mjini nd juma abdallah hamadi  amesema wameamua  kuangaluia  miradio hioyo ili kujiridhisha  ili kuona kama kuna mapungufu.

Hata hivyo katibu tawala huyo  ameswasihi wanachi kutoa mashirikiano   ya kutosha katika kufanikisha suala zima la taifa  ambalo linamaslahi kwa wana nchi wake.

Maeneo mengine yanayotarajiwa kupitwa na mwenge huo ni  sebleni,bavuai ambapo kutakuwa na ukabidhiswaji wa mwenge huo kwa vikosi vya zima moto, jeshi la polisi  makao makuu, pia utakwenda katika skuli ya jangombe msingi kuzindua ujengaji wa mabanda ya wanafunzi, skuli ya kidongo chekundu, mbalungini.

Aidha mwenge huo utaendelea na mbio zake katika maeneo ya ngome kongwe,makao makuu ya jku saateni na kumalizia mbio zake katika skuli ya chumbuni ambapo huko utahitimisha mbio zake kwa wilaya ya mjini ambapo utalala na siku inayofuata  ya julai pili utakabidhiwa  wananchi wa wilaya  ya magharibi ‘b’

Wananchi wanapendwa kutanabahishwa kuwa katika mkesha wa mwenge  huo  hali ya ulinzi na usalanma utaimarishwa  katika mazingira yote ya mkesha  huku wakitanabahishwa wananchi kujitokeza  kwa wingi  siku ya tarehe mosi july na usiku wake.

Mwenge huo  unatarajiwa  kukimbizwa kwa muda wa siku saba kwa unguja na  pemba utarajiwa kuzindua jumla ya miradi  30  kwa ungija na pemba .