MELI YA KITALIII YA NCHINI MISRI IKIWA NA ABIRIA MIA TISA IMEWASILI BANDARINI ZANZIBAR

 

Meli ya kitaliii ya bouccar ya nchini misri ikiwa na abiria mia tisa imewasili bandarini zanzibar kwa ajili ya kutembelea vivutio mbali mbali vya kitalii.  Akizungumza na waandishi wa habari mkurugenzi  masoko wa kamisheni ya utalii ndugu miraji  ussi amesema kuja kwa meli hiyo kutasaidia kuinua uchumi na pia wajasiriamali   watapata fursa ya kuuza bidhaa zao kwa wingi.

Naye afisa  habari  wa kamisheni hiyo ndugu  amour mtumwa  amesema  watalii hao wanatarajia kutembelea maeneo mbali mbali ambapo watasaidia kuitangaza zanzibar kibiashara kutokana na kuwa na vivutio vingi