MELI YA MV MAPINDUZI KUKAMILIKA KWA MATENGENEZO YAKE.

Mkurugenzi mkuu muendeshaji wa shirika la meli zanzibar nd salum ahmada vuai amesema jitihada za makusudi zilichuliwa ili kuhakikisha meli ya mv mapinduzi iliyoharibika moja ya mashine zake imetengenea mapema.
Meli hiyo iliharibika wakati ikiwa katika safari yake ya kawaida kuelekea pemba mwezi uliopita.
Amesema kufanikiwa kwa matengenezo hayo kumetokana na msaada wa kitaaluma kutoka kampuni ya damen ya holand na itaanza safari zake leo usiku
Fundi mkuu wa meli hiyo ramadhani mwinyi amewatoa hofu wananchi kutokuwa na wasi wasi juu ya usafiri wa meli hiyo na itaendelea na safari zake kama kawaida.
Katibu mkuu wizara ya ujenzi na mawasiliano mustafa aboud ameitembelea meli ya mv mapinduzi baada ya kukamilika kwa matengenezo yake.
Meli hiyo yenye uwezo wa kuchukuwa abiria na mizigo iliharibika moja ya mashine zake na kusababisha kutofanya kazi .