MELI YA UTAFITI WA UTAFUTAJI MAFUTA NA GESI ASILIA IMEMALIZA KAZI YAKE KATIKA KITALU CHA PEMBA-ZANZIBAR

 

Meli ya utafiti wa utafutaji mafuta na gesi asilia imemaliza kazi yake katika kitalu cha Pemba-Zanzibar na kuyafikia maeneo yote yaliyokusudiwa.

Meli hiyo ambayo ilianza kazi ya utafiti kwa mitetemo katika miamba baharini mwishoni mwa mwezi oktoba imemalizika tarehe 28 novemba ambapo jumla ya mistari 62 imefikiwa ndani ya kitalu hicho na kwa jumla zoezi hilo lilikuwa la mafanikio.

Mkurugenzi mwendeshaji mamlaka ya udhibiti wa utafutaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar Omar Zubeir amesema matokeo ya utafiti huo yatatolewa baada ya kukamilika zoezi la utafiti katika maeneo ya nchi kavu linalotarajiwa kuanza muda mfupi ujao.

Aidha Mkurugenzi huyo amesema wakati wa utafiti huo kulijitokeza matatizo kadhaa ikiwemo wavuvi kukatiwa nyavu zao lakini watalipwa fidia kutokana na uharibifu huo.

Kuhusu kazi ya utafiti maeneo ya nchi kavu amewatoa hofu wananchi kutokuwa na wasiwasi kwani hakutakuwa na madhara yoyote.