MFUKO WA HIFADHI YA JAMII YAKABIDHI MSAADA TUMBATU

 

 

Mfuko wa hifadhi ya jamii imekabidhi msaada wa miti na misumari ya kujengea yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano kwa waathirika wa upepo katika kisiwa cha tumbatu uliotokea mwezi julai mwaka huu.

Utoaji wa msaada huo ni sehemu ya  shamra shamra za sherehe za kutimia miaka 20 ya kuanzishwa mfuko huo.

Akikabidhi msaada huo meneja  huduma kwa wateja nd: filfil thani amesema mfuko upo karibu na jamii katika kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo elimu,afya na watu wenye mahiataji maalum na wameamua kuwasaidia waathirika hao kutokana na mchango wao kwa jamii .

Aidha  amewahimiza wanaostahiki michango katika mfuko huo  kujisajili na kukamilisha michango yao ili  kuijengea uwezo zssf ya kutoa misaada kwa jamii.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya kaskazini  “a” fakii kombo fakii amesema msaada huo umefika kwa wakati  hivyo watawapatia waathirika hao ili waweze kurudi katika hali yao ya kawaida na kuwaomba watu na taasisi nyengine kuwasaaidia waathirika hao.

Kwa upande  wao wakaazi wa kisiwa hicho wamewashukuru zssf kwa kutoa msaada huo kwani utawawezesha kurudisha makaazi yao kama kawaida.