MFUMO MPYA WA UDAHILI UTASAIDIA KUPUNGUZA WANAFUNZI WASIOKUWA NA VIGEZO

Mfumo mpya wa udahili kupitia mitandao utasaidia kupunguza tatizo la wanafunzi wasiokuwa na vigezo  kujiunga na vyuo vilivyo sajiliwa nchini.

Akizungumza katika mafunzo kwa maafisa udahili wa vyuo vilivyosajiliwa na baraza la taifa  la mitihani  (nacte), mkuu wa kanda ya  zanzibar Halima  Mbilinyi, amesema hatua hiyo itarahisisha kuwatambua wanafunzi wasiokuwa na sifa kwa kutowafanyia   usajili.

Amesema jukumu la baraza hilo ni kuendeleza na kuimarisha elimu ya ufundi kwa kusimamia shughuli za mitaala hivyo mabadiliko hayo  ni njia  bora za  ambazo zitasaidia kuvipa hadhi vyuo  vinavyosimamiwa  na  nacte.

Akifafanua kuhusiana na faida za kuanzishwa mfumo huo wa usajili wanafunzi kwa njia ya matandao, halima amesema utasaidia kupunguza gharama za ufatiliaji wa taarifa za kujiunga na vyuo kutokana na kupatikana moja kwa moja kupitia mtandao.

Washiriki wa mafunzo hayo wamesema mfumo huo ni mzuri na utaweza kuondoa udanganyifu  na urasimu hivyo wanafunzi wanapaswa kuwa makini ili kuepuka kujiunga na vyuo ambavyo havitambuliki.