MFUMO WA MAEGESHO YA MAGARI MANISPAA YA MJI WA ZANZIBAR

 

 

Baadhi ya madereva na watumiaji wa barabara wamesema mfumo wa maegesho ya magari katika maeneo ya manispaa ya mji wa zanzibar inachangia usumbufu wa matumizi ya usafiri wa barabara.

Wamesema ukosefu wa maegesho maalum hali inayosababisha kuruhusiwa vyombo vya moto hasa gari kuegesha pembezoni mwa barabara ambako sehemu neyngine hakuruhusiki kisheria ndio chanzo kikuu cha tatizo hilo na ajali zisizitarajiwa.

Zbc imetembelea katika baadhi ya meneo ambayo mara nyingi yamekuwa na msongamno na kusababisha foleni ikiwemo  mlandende, michezani na darajani ambapo baadhi ya wananchi wameelezea ugumu wanaoupata barabarani.

Malalamiko hayo yalifikishwa kwa mkuu wa maegesho wa baraza la manispaa ibrahimu maabadi ambae amesema wanaendelea na mpango maalum wa kuondosha maegesho yasiyo rasmi katika mji wa zanzibar.