MFUMO WA USIMAMIZI WA RASILIMALI ZISIZOHAMISHIKA KUPATIWA NJIA MBADALA

https://youtu.be/7dMgGWTdFVk

 

 

Serikali ya  mapinduzi  ya  zanzibar imo  katika  maandalizi  ya  mfumo  wa  usimamizi  wa rasilimali  zisizohamishika   ikiwemo  mchanga  katika  kutafuta  njia  mbadala  ili  kukidhi  mahitaji  ya  wananchi  wake.

Hali  hiyo  imebainishwa  katika  ziara  ya  kuyakagua maeneo  ya  rasilimali hizo naibu  waziri  wa  kilimo   maliasili  mifugo  na uvuvi  dk  makame  ali  ussi amesem ahivi  sasa  wamo  katika  kupanua  wigo  wa upatikanaji  wa rasilimali  nyengine   katika  ujenzi  ili  kuiweka  ardhi  katika  mazingira  salama.

Amefahamisha  kuwa umefika  wakati  wa  kuangalia  njia  mbadala  wake katika  ujenzi  baada  ya  mchanga  kutumika   vumbi  la  kokoto katika  utengenezaji  wa  matofali na  kuwa  wabunifu  wa  utengenezaji  wa  matofali  ya  matundu  ili  kupunguza  matumizi  ya mchanga.

Mkuu  wa  kitengo  cha  maliasili  zisizorejesheka  ngwali   makame  haji  amesema hali  ya  udhibiti  wa  rasilimali  hiyo  inahitajika ili  kuweza  kuendelea  kuwa chini  ya  serikali  ili  kupunguza  uharibifu  mkubwa  unaofanyika  pasi  na  kuangalia  hatma  ya  baadae  dhidi  ya  mazingira  ya  kisiwa katika  kujikinga  na  majanga  mbali  mbali  ikiwa  pamoja  na  nchi  kuwa  jangwa.

Nao  wafanyakazi  wa maeneo  hayo  ya uchimbwaji  wa  mchanga  yaliopo  pangatupu  wameiomba  serikali  kuwasogezea  maeneo  karibu  ya  ulipiaji  wa kibenk  juu ya  upatikanaji  wa  huduma  ya  mchanga  ili  kupunguza  msongamano  kama  uliopo  hivi  sasa.

Mapema uongozi  wa  wizara  ya  kilimo  maliasili  zisizorejesheka  kwa  kushirikiana  na  idara  ya  misitu ulikagua  eneo  la  donge  chechele  ambalo  lenye  mchanga mweupe  liko  ukingoni  kumalizika na  pangatupu  ambalo  linajumla  hekta 135 linaloendelea  na harakati zauchimbwaji wa mchanga.