MFUMUKO WA BEI UMESHUKA KUTOKA ASILIMIA 1.5

 

Mfumuko  wa  bei  umeshuka  kutoka asilimia 1.5  ya   mwezi   may  hadi   kufikia  asilimia 0.7 ya mwezi  june kutokana  na  upatikanaji  wa  bidhaa za kutosheleza  mahitaji  ya  wananchi.

Mkuu  wa  kitengo  cha  takwimu  za  bei  wa  ofisi  ya  mtakwimu  mkuu  wa serikali ndugu khamis  abdulrahman  msham amesema  hali  hiyo  imechangia  kushuka  kwa bidhaa  mbali  mbali  kutokana na kupatikana kwa wingi.

Amefahamisha  kuwa  bidhaa  za  chakula  na  vinywaji  visivyo  na  kileo  imeshuka  na kufikia  asilimia  1.0  kutoka  3.8  ukiwemo  mchele  wa  mbeya  kufikia  asilimia  2 nukta  4 sembe 2 nukta 0 na sukari 2 nukta 0 .

Mhadhiri  wa uchumi  kutoka  chuo kikuu  cha  taifa suza  dk suleiman msaraka  amesema hali  ya  uzalishaji  wa  bidhaa  za  chakula  kuwa  nzuri  imechangia  kushuka  kwa  kasi  ya  mfumuko  wa  bei  za  bidhaa  za  chakula nchini.

Meneja  msaidizi  benk  kuu  tawi  la  zanzibar moto  ngwinganele lugobi amesema  bado  hali  ya  uchumi  ipo  katika  tarakimu  moja kama  serikali  ilivyopanga  hivyo ipo  haja  kwa  sekta  husika  kuhamasisha  kilimo  ili  kutoa  unafuuu  wa  kasi  ya  mfumuko  wa  bei  za  bidhaa  nchini.