MFUMUKO WA BEI UMESHUKA KWA ASILIMIA 0.1 KWA MWEZI WA JULAI

 

 

Hali  ya  mfumuko  wa  bei  umeshuka  kwa  asilimia  0.1  kwa  mwezi  wa  julai  ukilinganisha  na  mwezi  june  2018  huku  ukionesha  kuongezeka  kwa  mwaka  kutoka  asilimia  3.5  hadi 3.9 kufikia  julai  2018   kutokana  na  kupanda  kwa  bei  za  mafuta  ulimwenguni.

Akitoa  taarifa  kwa  vyombo  vya  habari   mkuu  wa  kitengo  cha  takwimu  za  bei kutoka  ofisi  ya  mtakwimu  mkuu  wa  serikali  khamis  abdulrahman  msham  amesema  hali  hiyo ya  kushuka  kwa  bidhaa  za  chakula  kwa  mwezi kunachangiwa  kwa kuwepo kwa  bidhaa  kwa  wingi  sokoni na  kukidhi  mahitaji  ya  watumiaji.

Amefahamisha  kuwa  hali  ya  uzalishaji  wa bidhaa  za  chakula  imeongezeka  na kupunguza  kasi  ya  mfumuko  wa  bei  ambapo kumechangia  kushuka  kwa  bidhaa tofauti za  chakula  ikiwemo  mchele  kwa  asilimia  0.4 sembe 2.3 ngano 0.4sukari 9.7 na samaki 3.2.

Dk  suleiman  msaraka  kutoka  chuo  kikuu  cha  taifa  suza kwa  upande  wa  uchumi  amesema  hali  ya  uchumi  iko  vizuri  kutokana na kuwepo  katika  tarakimu  moja   hali  ya  kupanda  na  kushuka  kwa  mfumuko  wabei  ni  dalili  inayoonesha kuwa soko  huria  linafanya  kazi.

Meneja  msaidizi  kutoka   idara  ya  uchumi  kutoka  bank  kuu  kwa  upande  wa  zanzibar  deogratias macha  amesema  hadi  sasa hali  ya  uchumi ipo  vizuri  kutokana  na wananchi  kuwa  na  bidii  katika  uzalishaji  wa  bidhaa  za  chakula  kulikochangia  kupunguza  hali  ya  uagiziaji   kutoka  nje  ya  nchi.