MH CASTICO AMEZINDUA BODI YA MFUKO WA UWEZESHAJI WANANCHI KIUCHUMI.

Waziri wa kazi, uwezeshaji, wazee vijana wanawake na watoto mh. Modline cyrus castico amezindua bodi ya mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi.
Akizungumza na wajumbe wa bodi hiyo amewataka kuhakikisha mfuko unawafikiwa wananchi wengi zaidi hususani vijijini na walio katika makundi maalum.
Amewataka kutoa miongozo ya kazi ya kuendesha mfuko huo ili kufikia malengo.
Akizungumza na zbc baada ya uzinduzi huo mkurugenzi idara ya mikopo suleiman haji ali amesema mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi umeshatoa mikopo elfu moja mia mbili na tisa yenye thamani ya shilingi ya zaidi ya biliono mbili kwa unguja na pemba.
Bodi hiyo ina wajumbe saba chini ya mwenyekiti wake salim said bakheresa.