MH CHUMU KOMBO KHAMIS AMEWATAKA WANANCHI KUWA NA TABIA YA KUTEMBELEA MAENEO YA KIHSTORIA

 

Katika kuendeleza  mpango wa kuyatunza na kuyarejeshea  hadhi yake majengo ya kihistoria naibu waziri wa habari utalii na mambo ya kale  Mh Chumu Kombo Khamis  amewataka wananchi kuwa na tabia ya kutembelea maeneo ya kihstoria kwa lengo lakuyaenzi maeneo hayo.

Kati ya magofu ya kihistroria mbayo yanafanyiwa matengenezo makubwa ni kwa bi khole bungi ambapo naibu wazi wa habari, utalii na mambo ya kale mh chumu kombo, alipokuwa katika  ziara maalum ya kuangalia hatua ya ujenzi inayoendelea amewataka wakaazi wa maeneo hayo na vijiji jirani kujenga utamaduni wa kutembelea maeneo ya kihistoria ili kufahamu mambo muhimu ya kale.

Maeneo mengine aliyotembelea akiongozana na mkurugenzi wa makumbusho Nd. Salum Kitwana Sururu ni  magofu ya mwinyi mkuu dunga maarufu jumba la mawe ambalo lilmo katika matengenezo, lakini pia ametembelea  magofu yaliyopo  fukuchani.

Mh Bi Chum amesema mbali na majengo hayo kuwa ya kihistoria lakini ni muhimu katika kuimarisha sekta ya utalii hivyo serikali ipo katika mpango wa kuyadumisha kwa kuyafanyia matengenezo  na kuyarudishia hadhi yake.

Wakati huo huo, uongozi wa wizara ya habari, utalii na mambo ya kale umekagua maendeleo ya ujenzi katika nuymba ya zamani ya kulelea watoto forodhani, ambayo itatumika kwa kuhifadhiwa vifaa vilivyokuwemo katika makumbusho kuu ya beit el jaib ambayo inafanyiwa matengenezo makubwa,

Kamanda wa kikosi cha kmkm kinachofanya  ujenzi katika nyumba ya watoto ya zamani cdr haji mohamed amesema anaelezeahatua iliyofiwa ya ujenzi huo.