MH HAMAD RASHID AKIKABIDHI MAJENGO YA KUHIFADHIA DAWA KATIKA HOSPITALI YA MNAZIMMOJA

 

Wizara  ya  afya  zanzibar  imesema itamchukulia  hatua  za  kisheria   na  kumfukuza  kazi  mfanyakazi  yeyote  ambae   atahusika  kuuza  dawa  za  serikali zikiwemo  mali pamoja  na  kuwatolea  lugha  chafu  wagonjwa  wanaofika  kupata  huduma  katika  hospitali  na vituo  vya  afya.Waziri  wa  afya  mh  hamad  rashid muhamed ameeleza  hayo wakati  akikabidhi  majengo  ya  kuhifadhia  dawa    katika  hospitali  kuu  ya  mnazimmoja   yaliogharimu  zaidi  ya  milioni mia  sita yaliofadhiliwa  na  mfuko  wa fedha wa  dunia  global  fund.Amesema  ameweza  kugundua  kuwa   baadhi  ya  maduka  makubwa  ya  dawa  yanauza  dawa  zaserikali  zikiwemo  za  kutibu  malaria   pamoja na  za  uzazi  wa  mpango   na  baadhi  ya  wafanyakazi  kutumia  lugha  chafu  kwa  wagonjwa  jambo ambalo  ni  kinyume  cha  sheria.

Amefahamisha  kuwa  serikali  inatoa  pesa  nyingi   kwa  ajili  ya  kununulia  dawa   kwa  lengo  la  kuhudumia  wananchi   hivyo  amewataka watendaji  wa  hospitali  ya mnazimmoja  kuhakikisha  kuwa  wanapanga   mipango  madhubuti    ya uwekaji  wa  takwimu  sahihi   ili  kuweza  kuagiza  dawa  kwa  mahitaji  ya  wagonjwa.Mkurugenzi  wa  bohari  kuu  ya dawa zahrani  ali  hamad   amesema ameona  ipo  haja ya  kujenga  jengo   la kuhifadhia  dawa   kwa  hospitali  kuu   ya  mnazimmoja   kutokana  na  kuwa  mahitaji  yake  ni  makubwa  na sehemu waliokuwa  wakihifadhia  hapo  mwazo  haitoshelezi.Nae  mkurugenzi  mtendaji   wa  hospitali  ya  mnazimmoja   dk  ali  salum   ali   amesema  atahakikisha  wanaandaa   mfumo  mzuri  wa  upatikanaji  wa  dawa   kwa  wagonjwa    na  zinafikia  walengwa  kwa vile  serikali  ya  mapinduzi ya  zanzibar   inatil