MH ISSA GAVU AMESIFU MUITIKIO WA WANA DIASPORA KATIKA MASUALA MBALIMBALI YA NCHI ZAO

Waziri wa nchi afisi ya rais mh issa gavu amesifu muitikio wa wana diaspora katika masuala mbalimbali ya nchi zao hasa kwa ushiriki wao mzuri katika makongamano yanayoandaliwa.
Mh. Gavu akizungumza na waandishi wa habari amesema serikali imepata faraja kuona idadi kubwa ya wanasiapora kuonesha nia ya kushirikiana na serikali kusaidia masuala ya kijamii na hata ya taifa.
Hata hivyo amesema mafanikio hayo yanatokana na ushirikiano wa wananchi pamoja na kuzishajihisha taasisi binafsi na serikali kufanikisha suala hilo.
Aidha waziri gavu amesema serikali itaandaa utaratibu mzuri wa kutambua kiwango cha fedha kinachotumwa na diaspora kwa familia zao ili kuona ni kwa kiasi gani zinavyoweza kuchangia pato la taifa