MH MAJALIWA AMEWATAKA VIONGOZI WABORESHE MIUNDOMBINU YA VIWANDA

Waziri mkuu kassim majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa pwani waboreshe miundombinu ya maeneo waliyoyatenga kwa ajili ya ujenzi wa viwanda ili waweze kuwavutia wawekezaji wa nje na ndani.
Ametoa agizo hilo wakati akizungumza na kwa nyakati tofauti na wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneza sabuni ya unga cha keds kilichopo kibaha na kiwanda cha kutengeneza vigae cha twyford kilichopo chalinze.
Waziri mkuu amesema ameridhishwa na kasi ya maendeleo ya ujenzi wa viwanda mkoani pwani na amewaagiza viongozi wahakikishe maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji yanakuwa na miundombinu muhimu kama maji, umeme na barabara.
Awali, mkurugenzi mtendaji wa viwanda hivyo bw. Jack feng amesema ujenzi umekamilika kwa asilimia 90 na vinatarajiwa kuanza uzalishaji oktoba mwaka huu na amesema vigae vitakavyozalishwavitauzwa kwa gharama nafuu kutokana na asilimia 95 ya malighafi inapatikana ndani ya nchi..
Kwa upande wake, mkuu wa mkoa wa pwani, mhandisi evarest ndikilo amemuomba waziri mkuu awasaidie upatikanaji wa nishati ya umeme ya kutosha kuweza kuendesha viwanda katika mkoa huo.