MH MIHAYO AMETOA MUDA WA WIKI MOJA KUKAMILIKA UJENZI WA SOBER HOUSE KIDIMNI

 

Naibu waziri wa nchi ofisi ya makamu wa  pili wa rais mh mihayo juma nunga ametoa  muda wa wiki moja  kwa kampuni ya   al- hilal general trading kukamilisha ujenzi wa  nyumba za watu walioacha kutumia dawa za kulevya sober house zilizoko  kidimni wilaya ya kati.Akizungumza katika ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa nyumba hizo naibu waziri huyo amesema  ametoa uamuzi huo kutokana na kumalizika kwa muda wa mkataba waliokubliana  na kinachofuata sasa ni makubaliano ya kuwaongezea muda ili wakamilishe ujenzi huo.Fundi mkuu wa kampuni hiyo hemedi al- hilal  amesema   kazi  hiyo   ilitarajiwa kukamilika januari 11 lakini kutokana na kukosa mchanga wenye kiwango ndipo kazi hiyo ikachelewa.

Kazi ya ujenzi wa nyumba hizo za makaazi zilianza mwezi wa tano mwaka uliopita na kazi hiyo walipewa kampuni ya al- hilal  ambayo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho.