MH’ MOHAMED AHMADA AMEWATAKA WANAFUNZI WANAOTARAJIA KUFANYA MITIHANI YA KIDATO CHA NNE KUJIAMINI

 

 

mwakilishi wa jimbo la malindi ujenzi mawasiliano na Mh’ Mohamed Ahmada amewataka wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kidato cha nne kujiamini wanapofanya mitihani yao  ili waweze kufanya vizuri mitihani yao

mh mohamed ahmada ambae pia ni naibu waziri wa ujenzi mawasiliano na usafirishaji ameeleza hayo wakati akikadhi shilingi milioni nne kwa skuli nne za mkoa wa mjini magharibi kwa wanafunzi wanaokaa kambi za matayarisho ya mitihani hiyo.

nao wanafunzi  waliopokea msaada huo wamemtaka mwakilishi huyo kuendelea kuzisaidia skuli hizo kwa vile zinakabiliwa na matatizo mbali mbali.

skuli zilizopatiwa msaada huo ni skuli ya hamamni, hurumzi, forodhani na vikokotoni ambazo zinatarajiwa kufanya mitihani yao tarehe 5 mwezi huu