MHE. AYOUBU AMESEMA MKOA HUO UNAFARIJIKA NA MAENDELEO YA VYAMA VYA USHIRIKA

Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mhe. Ayoub Mohamed Mahmoud amesema mkoa huo unafarijika na maendeleo ya vyama vya Ushirika katika shughuli za zao za kila siku.

amesema mafaniko hayo yanasaidia katika kujiimarisha kiuchumi na kuweza kusaidia maendeleo ya masauala mengine muhimukatika jamii.

akipokea Madawati kutoka Saccos ya Madereva wa Texi za uwanja wa ndege kwa ajili ya Skuli ya Kiembe Samaki Msingi a amewaomba wadau kusaidia sekta ya elimu ili kutatua matatizo mbalimbali ya sekta hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Wizara Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na watoto Khamis Daud Simba amesema Serikali itaendelea kuviendeleza vyama vya ushirika ili viendelee kufanya kazi vizuri.

mwenyekiti wa ushirika wa Madereva wa Taxi Uwanja wa Ndege Zanzibar Kassim Gharib Makame amesema wameamua kutoa msaada huo ikiwa ni juhudi za kuendeleza sekta ya elimu Zanzibar.

 

nae diwani mstaafu wa wadi ya kiembesamaki gharibu ameahidi kushirikiana na wafadhili mbali mbali katika kuhakikisha wanachangia madawati mia moja kwa ajili ya maendeleo ya vijana wao na skuli ya Kiembe Samaki kwa mssada uliotolew na ushirika wa Uwanja wa Ndege umewasukuma na kuona wana dhima ya ya kusaidia Skuli hiyo.