MICHUANO YA GOLF ZANZIBAR MWAKA 2017 INATARAJIWA KUFANYIKA MAPEMA MWEZI UJAO

 

Michuano  ya golf zanzibar  mwaka 2017 inatarajiwa  kufanyika mapema mwezi ujao   katika viwanja  vya hoteli ya sea clif kiomba mvua  na kushrikisha wachezaaji kutoka ndani na nje ya nchi

Akizungumza na waandishi wa habari mratibu wa mashindano hayo kutoka klabu ya rotary zanzibar bi sjani muggenburg  amesema matayarisho yote kwa ujumla  yamekamilika ikiwemo vifaa vya mashindano pamoja na  wanachokisubiri sasa ni mchakato wa kuwapata  idadi ya washiriki katika michezo hiyo

Mkurugenzi wa zanlink bw san jay raja mesema kwa mwaka huu  mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika terehe 4 november 2017.ambapo  hadi kufikia sasa wanamichezo mbalimbali kutoka ndani  na nje ya tanzania  watashiriki katika michezo hiyo.

Nae katibu wa golf zanzibar  issa chap  amesema kwa upande wao wanaishukuru  rotary club kwa mchango wao na kwamba wamejiandaa  vizuri   na mashindano hayo kwani ni njia moja  wapo  ya kuipa kipaumbele  michezo hiyo  na kuifanya  iwe na hadhi  zadi  zanzibar  na tanzania kwa ujumla.