MICHUANO YA LIGI YA MPIRA WA KIKAPU IMEENDELEA TENA NA MBIO ZAKE KATIKA KIWANJA CHA MAISARA

Michuano ya ligi ya mpira wa kikapu imeendelea tena na mbio zake katika kiwanja cha maisara kwa maafande wa polisi kutoa kipigo cha points 68 dhidi ya cavarias waliopata points 40 katika pambano lililopigwa wakati wa mchana.
Ligi hiyo hiyo inazishirikisha timu 14 na inatarajiwa kutia nanga mwanzoni mwa mwezi ujao.
Akizungumza na zbc mdhamini wa michuano hiyo hamid suleiman amesema timu ya mbuyuni iko katika nafasi nzuri baada ya jana kuibuka na points nyingi.
Amekishauri chama cha mpira wa kikapu kuwashajiisha vijana zaidi kujiunga na timu za mchezo huo ili uweze kuwa na mashabiki wengi zaidi.
Katika mchezo ulipigwa jioni hii rangers wamewatandika betras kwa points 71 kwa 47 katika pambano lililokuwa na upinzani mkali.