MIEZI SITA YA UTOWAJI WA HUDUMA ABDALLAMZEE HOSPITAL

Uongozi wa hospitali ya abdalla mzee mkoani umesema umethubutu kutoa huduma za matibabu ya afya kwa wananchi kutokana na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo dk. Haji mwita haji amesema wamekumbana na changamoto mbali mbali katika utowaji wa huduma kwa wananchi kwani walipokuwa napewa ushauri wa kimatibabu na wafanyakazi walishindwa kuuamini kutokana na ukubwa wa hospitali hiyo.
Uongzo huo umetowa kauli hiyo kwenye kikao cha kupongeza cha wafanyakazi wa hopitali hiyo kwa kutimiza miezi sita ya utowaji wa huduma katika hospitali tokea kufunguliwa na kukabidhi zawadi kwa wodi bora ya wazazi.
Aidha dk. Mwita ameitumia nafasi hiyo kuishauru wizara ya afya kuwapatia mafunzo hasa katika kitengo cha maabara ili wafanyakazi wavitumie vifaa litaalamu zaidi.
Akitowa nasaha zake katika kikao hicho afisa uendeshaji wa huduma za hospitali dk. Omar ali mbarawa amesema mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha miezi sita katika utowaji wa huduma za jamii yawe ni fursa za kukabiliana na changamoto za utowaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.