MIKOKO ELFU NNE NA MIKUNGU 30 IMEPANDWAKATIKA ENEO LA KILIMANI

Jumla ya mikoko elfu nne na mikungu 30 imepandwakatika eneo la kilimani ili kunusuru eneo hilo kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Akizungumza na wana jumuiya ya zacedi mtaalamu wa upandaji miti bwana mwita mwangora kutoka taasisi ya sayansi za bahari daresalaam amesema upandaji wa mikoko ni moja ya mbinu muhimu katika utunzaji wa fukwe pamoja na mazingira ili kuhakikisha eneo hilo linakua endelevu.
Ameongeza kwa k usema kua mikoko inatumika katika hatua ya ukuaji wa samaki pia ni rasili mali ya taifa hivyo ni vyema kwa wanajamii kuyatunza mazingira hayo.
Afisa mazingira wa zacedi bi hawa masoud ametoa wito kwa wananchi watunze mazingira kwani faida itakayopatikana ni kwa jamii.
Nae mwanajumuiya ndugu shija julius jamii isisubiri taasisi au serikali katika utunzaji wa mazingira bali wawajibike wao wenyewe bila kurutishwa.