MIKOKO NA MIKANDAA ELFU THALATHINI INATARAJIWA KUPANDWA

 

 

Zaidi  ya mikoko na mikandaa  elfu thalathini  (30,000)  inatarajiwa kupandwa  katika hekta  18 nukta 5 zilizoathirika na  maji chumvi katika  maeneo ya bonde  la tovuni, ukele na tumbe mashariki  katika wilaya ya micheweni.

Akizungumza na  zbc  mara ya kukaguwa maeneo hayo  katibu mkuu wizara ya ardhi,maji,nishati na mazingira  nd,alihalily mirzah  amesema  kutokana na uharibifu  huo  wizara imeamua kuwashirikisha wananchi  katika kuwapatia  elimu ya utunzaji wa  mazingira  na kuwashajihisha  katika upandaji  wa mikoko na mikandaa ili kukabiliana na hali hiyo.

Nae mkurugenzi  mkuu wa mamlaka ya usimamizi wa mazingira  nd,sheha mjaja juma amesema  programme  za kuwashirikisha wananchi zinaendasambamba na mkakati wa pili wa mbadiliko ya tabia ya nchi  wa kitaifa  ambao unahusika  kuwa na mpango  wa kijamii  unaolenga  katika kuhimili  na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi.

Mabadiliko ya tabia ya nchi  bado yamekuwa ni  changamoto katika uharibifu wa mazingira kutokana na  maji chumvi kuendelea kushambulia maeneno  mbali mbali katika kisiwa cha pemba.