MILLIONI MIA MOJA NA ARUBAINI NA TANO ZIMEPOTEA KUWALIPA WAFANYAKAZI HEWA

 

 

 

zaidi ya shilingi millioni mia moja na arubaini na tano zimepotea kutokana na kuwalipa wafanyakazi hewa 46 waliokuwa wakifanya kazi katika wizara ya elimu na mafunzo ya amali.

katik taarifa yake kwa waandishi wa habari katibu wa baraza la mapinduzi na katibu mkuu kiongozi dk abdulhamid yahya mzee amesema fedha hizo zililipwa wafanyakazi ambao wako likizo bila ya malipo, walioacha kazi na wagonjwa wa muda mrefu ambao hawaendi kazini.

amesema katika uhakiki uliofanywa na mdhibiti na mkaguzi wa hesabu umebaini kuwa fedha hizo zilikuwa zikiingizwa kwenye akaunti zao bila ya wafanyakazi hao kuwepo kazini.

baada ya serikali kuzifatilia fedha hizo kiasi cha shilingi milioni thamanini na mbili zimerejeshwa na wafanyakazi hao na kuwataka ambao wajarejesha kufanya hivyo haraka kabla hawajachukuliwa hatua za kisheria.

katibu mkuu huyo kiongozi ameongeza uwa serikali imewafukuza kazi wafanyakazi 28 waliochukuwa likizo bila ya malipo kwa muda mrefu na kuwastaafishwa kazi wafanyakazi 8 wagonjwa kwa muda mrefu.

 

hata hivyo amezitaka taasisi za serikali kufanya uhakiki wa wafanyakazi kila baada ya muda ili kuweza kuondoa udanganyifu katika mishahara.