MIRADI IMEGUSA MAENDELEO YA WANANCHI KUONDOSHA KERO

 

Taasisi zenye miradi itakayozinduliwa wakati wa maadhimisho ya kutimia miaka 54 ya sherehe za mapiduzi zanzibar zimetakiwa kuongeza juhudi ya kazi ili kukamilisha miradi hiyo.

Akizungumza katika ziara ya kukagua miradi hiyo mkuu wa mkoa wa kaskazini pemba mhe, omar khamis othman amesema serikali imeingiza miradi hiyo katika ratibaya maadhimiso hayo hivyo ni lazima imalizwe mapema ili iwahi sherehe hizo.

Amesema miradi hiyo imegusa maendeleo ya wananchi na kwamba  wanaisubiri kwa hamu kubwa iwaondoshee shida zao zikiwemo za afya ,mawasiliano na maji safi na salama .

Aidha amewataka madiwani masheha na watendaji wengine kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi wakati waufunguzi wa miradhi hiyo ili wajionee jitihada za serikali yao.

Wasimamizi wa miradi hiyo wamemuahidi mkuu huyo wa mkoa kwamba watakamilisha miradi hiyo kwa wakati muafaka.