MISAADA INAHITAJIKA KWA AJILI YA WATOTO WA ROHINGYA WALIOKIMBILIA NCHINI BANGLADESH.

 

 

Shirika la umoja wa mataifa linalohudumia watoto-unicef limetoa wito wa kutolewa haraka misaada ya kutosha kwa ajili ya watoto wa kabila la rohingya waliokimbilia nchini bangladesh.

Wakimbizi hao, wanahitaji haraka chakula, maji safi ya kunywa, chanjo, dawa na kupatiwa matibabu ya kiakili.

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa waislam laki sita wa jamii ya rohingya wamekimbia mateso nchini myanmar.

Mkutano wa wafadhili umepangwa kuitishwa jumatatu inayokuja mjini geneva kukusanya fedha kwa ajili ya wakimbizi hao.