MIUNDOMBINU NI TATIZO KUBWA KWA WATU WENYE ULEMAVYU

Upatikanaji wa haki za watu wenye ulemavu wa akili bado ni tatizo kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya mawasiliano baina yao na vyombo vya sheria.

Akizungumza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo polisi na watendaji wa mahakama mratibu wa jumuiya kwa watu wenye ulemavu wa akili Zanzibar Khamis Abdallah amesema jumuiya hiyo inachukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha wanapata haki zao.

Naibu katibu wa jumuiya hiyo Juma Salum amesema polisi na watendaji wa mahakama wanapambana na matatizo mengi katika utekelezaji wa kazi zao katika kuwapatia wanachi haki zao.

Washiriki wa mafunzo hayo wameeleza kuwa mfumo halisi wa sheria unavikwazo kwa watu wenye ulemavu kupata haki zao, hivyo wameomba kuwepo kwa ushirikiano kuanzia kwa wananchi hadi ngazi ya mahakama ili kuwasaidi kupata haki zao.