MJUKUU WA MALKIA WA UINGEREZA, PRINCE WILLIAM AMEWASILI NCHINI TANZANIA

 

Mjukuu wa malkia wa uingereza, prince william amewasili nchini tanzania kwa ziara maalum ya siku tatu ambapo kesho anatarajiwa kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa tanzania DK. JOHN MAGUFULI Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Prince William katika kukutana na Rais Magufuli atafanya mashauriano kuhusu juhudi zinazochukuliwa na Tanzania katika kukabiliana na ujangili na ulanguzi wa wanyama pori.

Prince William na ujumbe wake ambapo amepokelewa na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla, Waziri wa Katiba Sheria profeas Kabudi  pamoja na viongozi wengine akiwemo Balozi wa Uingereza hapa Nchini na Mabalozi mbalimbali.

Pamoja an kukutana na RAIS MAGUFULI Mwanamfalme huyo, anatarajiwa kutembelea bandari ya Dar es salaam katika kitengo cha Polisi Marine na maeneo ya kupokelea mizigo, upekuzi na ukaguzi wa vinavyoingia na kutoka katika eneo hilo la bandari.

Prince William atafanya ziara hiyo katika wadhifa wake kama rais wa mashirika yanayotetea uhifadhi wa wanyama ya United for Wildlife na Tusk Trust.

Amekuwa pia mlezi wa shirika la Royal African Society linalolenga kukuza uhusiano kati ya Afrika na Uingereza na hushiriki sana juhudi za kukabiliana na ujangili.