MKOA WA MJINI MAGHARIBI UMEBAINI WAHALIFU 336 WA MATUKIO TOFAUTI

Mkuu wa mkoa mjini magharibi mh ayoub mohamed mahmood amesema mkoa huo umebaini wahalifu 336 wa matukio tofauti katika mkoa huo ambao wanatakiwa kujisalimisha wenyewe katika vyombo vya dola.
Amesema wahalifu ha wanaotuhumiwa kuhusika kwa makosa ya kuvuja kuiba kupora na kujeruh watu kwa mapanga ambapo tayari taarifa zao zimeshapatikana.
akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali juu ya hali ya usalama wa matukio yanayotokea katika mkoa huo amesema watuhumiwa hao wanatoka katika shehia tofauti na kuwataka wazazi wa watu hao kuwapeleka wenyewe vituo vya polisi kwa maelezo zaidi.
Amesema serikali ya mkoa huo umeazimia kuondosha matatizo ya kihalifu na kuwatoa hofu wananchi kwamba mkoa huo upo salama.
Akizungumzia mikakati ya mkoa huo ni pamoja na mardi wa kuweka camera za cctv ili kubaini matukio yote mabaya ndani ya mkoa huo sambamba na kuseam wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa suala la matumizi ya madawa ya kulevya.