MKURUGENZI WA MASHTAKA ZANZIBAR ( DPP) AKIZUNGUMZA UWASILISHAJI WA RIPOTI YA UENDESHAJI WA KESI ZA UDHALILISHAJI

Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar ( DPP)  Nd.Ibrahim Mzee Ibrahim amesema tangu kuzinduliwa kwa operesheni ya uendeshaji wa kesi za udhalilishaji katika mahakama zote za Zanzibar kumeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kusikilizwa na kufanyiwa maamuzi  kesi hizo kwa muda mfupi ukilinganisha na hapo awali.

akizungumza katika uwasilishaji wa ripoti ya operesheni ya uendeshaji wa kesi za udhalilishaji mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ya Mkurugenzi wa mashataka iliyopo uwanja wa Matumbaku amesema,operesheni hiyo ya awamu ya kwanza iliyoanzia Tarehe 01.3.2017 imewezesha ofisi hiyo kupeleka Majalada 55 katika Mahakama mbali mbali za Unguja na hatimae kuwezesha kesi 53 kati ya hizo kusikilizwa na nyengine kutolewa hukumu ndani ya kipindi kifupi.

mbali na hilo mkuregenzi wa mashtaka amekemea baadhi ya makadhi wanaotoa vyeti feki vya ndoa kwamba kufanya hivyo ni kosa la jinai na kuwatahadharisha kwamba kuanzia sasa atakaebainika kufanya udanganyifu huo atashtakiwa kwa kosa la kuidanganya serikali.

aidha Dpp aliziomba taasisi zinazojishughulisha na haki jinai kuzidisha mashirikiano ya pamoja kama ambavyo wameanza kupitia operesheni  hizo maalum walizozianzisha ili kusukuma mwenendo wa kesi za udhalilishaji ziende kwa haraka ili kuona tatizo hilo linamalizika.

mkutano huo wa dpp na waandishi wa habari juu ya kutambulisha uzinduzi wa operesheni ya uendeshaji wa kesi hizo kwa awamu ya kwanza n ya pili umekenda sambamba na kuwataka wananchi kujitokeza kutoa ushahidi wa kesi za udhalilishaji kwani kwani bila ya ushahidi ofisi ya muendesha mashtaka haitaweza kupeleka majalada mahakamani na hatimae wananchi watailaumu serikali wakati wakosa ni wao wananchi