MKUTANO WA KILELE WA VIONGOZI WAKUU WA UMOJA WA AFRIKA UMEMALIZIKA LEO

 

Mkutano wa kilele wa viongozi wakuu wa umoja wa afrika, umemalizika leo ambapo ajenda kuu zilizojadiliwa zilikuwa ni rushwa na migogoro.Hapo jana rais wa halmashauri kuu ya umoja huo moussa faki mahamat amesema, wakati umewadia wa kuwawekea vikwazo  wanaozuwia kusimamishwa mapigano sudan kusini.Sudan kusini ni moja wapo ya masuala yaliyojadiliwa na viongozi hao wakuu katika mkutano wao huo wa mjini addis ababa.Juhudi za kufufua mkataba wa amani wa mwaka 2015, zimesababisha kupatikana makubaliano ya usimamishaji mapigano desemba mwaka jana, lakini yakadumu saa chache tu, huku kila upande ukiulaumu upande wa pili kwa kukiuka makubaliano hayo.Wakati huo huo katibu mkuu wa umoja wa mataifa antonio gutteres ameahidi kuunga mkono  umoja huo kwa hatua zozote za ziada zitakazochukuliwa na umoja wa afrika.