MKUTANO WA VIONGOZI WA UMOJA WA ULAYA MJINI BRUSSELS

 

Kansela angela merkel wa ujerumani amesema katika mkutano wa viongozi wa umoja wa ulaya mjini brussels, kuwa atafanya juhudi kuhakikisha mazungumzo ya kujitoa kwa uingereza katika umoja huo-brexit yanafanikiwa.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kufikiwa makubaliano na sio aina yoyote ya makubaliano ambapo maendeleo kidogo yamepatikana lakini  hayatoshi kuweza kuingia katika awamu ya pili ya mazungumzo ya brexit.

Suala la kujitoa uingereza katika umoja wa ulaya linatazamiwa kutawala katika mazungumzo ya viongozi wa umoja wa ulaya mjini brussels.

Wakati huo huo umoja huo wa ulaya unataka kuipunguzia uturuki msaada wa fedha zinazotolewa kwa ajili ya nchi inayojiandaa kujiunga na umoja huo.

Mjadala umezuka mjingoni mwa nchi za umoja huo kuhusu msaada wa fedha za umoja huo kwa uturuki ambao umesababishwa na kukamatwa waandishi wa habari na wanaharakati wa haki za binaadam nchini uturuki.