MKUU HUYO WA MKOA AMEMALIZA ZIARA YAKE KATIKA WA MALINDI ULIOWAKUTANISHA WAKAAZI WA SHEHIA 12

 

Mkuu wa mkoa mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohammed Mahmoud ameuagiza uongozi wa Baraza la Manispaa ya mjini idara ya utunzaji na uendelezaji barabara uub na kampuni ya zeco kuhakikisha wanaifanyia matengenezo barabara ya kwa biziredi misufini iliyo chimbwa kwa kupitisha waya wa umeme.

Mhe Ayoub ametoa agizo hilo katika mfululizo wa ziara zake za kuzungumza na wananchi  wa mkoa huo kusikiliza malalamiko ya wananchi na kusema ni vyema matengenezo hayo yakafanya ndani ya wiki moja kutokana na usumbufu unaowapata wananchi.

Amefahamisha kuwa barabara hiyo ina umuhimu mkubwa kama zilivyo nyingine na kwamba lazima iwe katika mazingira mazuri yatakayowawezesha watumiaji kutopata usumbufu.

Mkuu huyo wa mkoa amemaliza ziara yake katika wa malindi uliowakutanisha wakaazi wa shehia kumi na mbili na kuzungumzia kero zao.