MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI RWANDA

 

Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Igp Simon Sirro amekutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa jeshi la polisi nchini Rwanda igp Emanuel gassan jijini Dar es salaam.akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya jeshi la polisi nchini igp Sirro amesema katika mkutano huo wamekubaliana kushirikiana katika kudhibiti uhalifu wa mapakani pamoja na kubadilishana uzoefu..

Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi nchini Rwanda igp Emanuel Gassan amesema makubaliano hayo ni mwendelezo wa ushirikiano baini ya nchi hizo mbili.