MKUU WA WILAYA YA KASAZINI ‘B’ AMEONYA WANANCHI WAKIWEMO WAJASIRIAMALI WASIOTII SHERIA

 

Mkuu wa wilaya ya kasazini ‘b’  ndugu issa juma ali ameonya wananchi wakiwemo wajasiriamali wasiotii sheria na kudharau viongozi wa shehia.

Amewataka wananchi wenye tabia hiyo kuacha  vyenginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Mkuu huyo wa wilaya ametoa onyo hilo  alipokuwa akizungumza na wajasiriamali wanaofanya shughuli  mbalimbali katika diko la mangwapwani.

Amesema  serikali imeweka sehea katika kuendesha shughuli mbalimbali ambapo wananchi wanapaswa kuzifuata .

Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, afisa wa uhamiaji inspekta saleh abass moh’d na afisa wa kikosi maalum cha kuzuia magendo(kmkm) luteni  abdulwahid abeid khamis wamewataka wajasiriamali wa diko hilo na madiko mengine kutowa taarifa za maafa,usafirishwaji wa bidhaa kimagendo na wahamiaji haramu ili  vikosi vya ulinzi vifanye kazi zake.

Afisa sheria wa halmashauri ya wilaya ya kaskazi B Asya Moh’d Mzee na Mkurugenzi wa halmashauri hiyo bi.fatma moh’d juma wamesema kuanzia mwenzi  ujao watahakikisha biashara  zote zinalipiwa kodi zinazostahiki.

Nao wajasiriamali wa diko la mangapwani wametowa malalamiko juuya  huduma za kijamii pamoja na kushauri mambo kadhaa yafanyike katika kuimarisha huduma.