MKUU WA WILAYA YA KASKAZINI B AMESIMAMISHA UJENZI WA NYUMBA KATIKA ENEO LA MWEMBE HEMARI

 

mkuu wa wilaya ya kaskazini b nd rajab ali rajab amesimamisha ujenzi wa nyumba zinazojengwa katika eneo la mwembe hemari  shehia ya gube  hadi  ofisi yake itakapojiridhisha kuhusu taratibu za ujenzi na uuzaji wa viwanja katika eneo hilo.

agizo hilo amelitowa  alipofika katika eneo lililokatwa viwanja na kujengwa nyumba ambalo limekuwa likitiliwa mashaka kuwa ni eka.

amesema maeneo mbali mbali yamekuwa yakifanywa ukataji wa viwanja na ujenzi wa nyumba bila ya kufuata sheria hivyo eneo hilo limesitishwa kwa kuebndelea na ujenzi wowote.

aidha wamewataka wananchi kuacha tabia ya kuuziana viwanja bila ya kuishirikisha serikali kwani inaweza ikasababisha migogoro ndani ya jamii.

sheha wa shehia ya kwa gube khamis makame ali amesema wanajitahidi kuwafahamisha wananchi juu ya kufuata utaratibu wa mauzianao ya viwanja na wao hawajishughulishi katika masuala hayo.

hata hivyo wanafamilia ya bw haji hamdani wamesema eneo wanalolijenga ni shamba na  wamerithi kutoka kwa baba yao na wala hawajauza isipokuwa wamekatiana viwanja wenyewe kwa wenyewe.

 

Comments are closed.

Powered by Live Score & Live Score App