MKUU WA WILAYA YA MKOANI AMEZINDUA UVUNAJI WA ZAO LA VITUNGUU

Uvunaji wa zao la vitunguu katika shamba darasa shehia ya mjimbini mkuu wa wilaya ya mkoani hemed suleiman abdalla amezindua wilaya ya mkoani ambalo limewahusisha wanajamii walio katika mradi wa kunusuru kaya masikini kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii tasaf .
Akizindua uvunaji huo amesema shamba hilo limekuwa ni taaluma kwa wananchi kwani hapo awali watu walidhani kwamba mazao kama vitunguu, pilipili boga, matikiti kwa kisiwani pemba hayawezi kukubali kutokana na kuwa walikuwa hawajawahi kulima kilimo hicho.
akielezea malengo ya tasaf ya kutoa ajira za muda kwa walengwa walio katika mpango wa kuzinusuru kaya masikini mratib wa tasaf pemba mussa said amesema
Akizungumzia mafanikio ya kilimo hicho bwana shamba wa shehia ya mjimbini amini rashid mdowe amesema pamoja na changamoto zilizojitkeza za uwepo wa mvua nyingi kwa msimu uliopita lakini kilimo hicho kimeonesha kukubali na kuwataka wakulima wa eneo hilo kukiimarisha hasa kwa vile hakitumii gharama kubwa katika kukiendeleza.
Kwa upande wao wakulima hao ambao niwalengwa wa mradi wa kuzinusuru kaya masikini wamesema wanaishukuru tasaf kwa kuwapatia elimu hiyo na kuahidi kukiendeleza kilimo hicho ili iwe ni sehemu ya zao la biashara na kuweza kuondokana na hali ya umasikini.