MLANDEGE SPORT CLUB IMEIBUKA KIDEDEA DHIDI YA MALINDI

 

Mlandege sport club imeibuka kidedea dhidi ya malindi katika mchezo wa bonanza la kuadhimisha sitini na moja tokea kuanzishwa kwa ujamaa sport club.

Mchezo uliopingwa jioni ya leo katika dimba wa amani mchezo ambapo umeweza kuibuwa hamasa kwa watazamaji wa visiwani hapa.

Mchezo huo uliokuwa wavutia wapenzi wa soka hapa visiwani pamoja na shangwe za wapenzi wa timu zote mbili mlandege walifanikiwa kuandika bao kipindi cha kwanza.

Malindi waliovalia jezi rangi nyeusi kwa wekundu walionekana kulishambulia goli la mlandege katika muda wote bila ya mafanikio.

Mara baada ya mchezo kumalizika zbc michezo ipata kuzungumza na walimu wa timu zote mbili mwalimu wa malindi saleh machupa amesema kipigo hicho hakija muathi kwa kuwa timu yake ipo katika maandalizi ya ligi kuu ya zanzabar.

Kocha wa mlandege amejinasibu kwa kusema mashirikiano na kufata maelekezo ya mwalimu ndio chachu ya ushindi huo.

Bonanza hilo la kuadhimisha miaka sitini ya ujamaa inatarajiwa kumaliza tarehs ishirini na mbili katika dimba la uwanja wa amani ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa makamu wa pili wa rais balozi seif ali iddi.