MORGAN TSVANGIRAI AMEFARIKI DUNIA

 

Msemaji wa chama cha -viguvugu la mageuzi ya kidemokrasi – mdc – nchini zimbabwe amethibitisha habari za kifo cha kiongozi wa muda mrefu wa upinzani, nchini humo morgan tsvangirai.

Tsvangirai akiwa na umri wa miaka 65 alikuwa akiugua maradhi ya saratani ya utumbo na alikuwa akitibiwa nchini afrika kusini.

Licha ya hali yake, morgan tsvangirai alipanga kugombea kiti cha urais, wakati uchaguzi utakapoitishwa baadaye mwaka huu.

Tsvangirai alikuwa hasimu mkubwa wa kisiasa wa rais wa zamani robert mugabe ambapo aliingia katika uwanja wa kisiasa kupitia vyama vya wafanyakazi.

Mwishoni mwa miaka ya 90 aliunda chama chake cha vuguvugu la mageuzi ya kidemokrasi – mdc, ingawa hakupata nafasi ya kuleta mageuzi ya kisiasa.

Baada ya uchaguzi mwengine uliokumbwa na visa vya udanganyifu mwaka 2008 na baada ya miezi kadhaa ya vurugu, tsvangirai aliwahi kukabidhiwa wadhifa wa waziri mkuu na rais robert mugabe, katika serikali ya umoja wa taifa.