MOTISHA KAZINI NI VIGEZO VINAVYOZIDISHA UFANISI WA KAZI

 

Suala  la  motisha  kazini  ni  miongoni  mwa   vigezo  vinavyowajenga wafanye kazi  kwa ufanisi  sambamba  na  kutekeleza  vyema  majukumu  yao  ili  kujengeka  taifa  lililojiimarisha   kielimu.

Mkuu wa  divisheni wa  kituo  cha  walimu  cha  taifa  mwalimu  maulid  omar akizungumza wakati wa  kuagwa  walimu  wakuu  nane  wa  kituo  cha  walimu  bububu amesema   ni wajibu  wa kuhakikisha  wanaendana  na  mfumo  wa elimu  uliopo  ili  kuwawezesha  wanafunzi  kuongeza  kasi ya  ufaulu.

Katika  risala  yao  walimu  wa  kituo  hicho  wameomba   kutatuliwa  changamoto  zilizopo  kituoni  hapo  ikiwemo  suala  la  upungufu wa  computer  na  umalizikaji wa vyoo  ili  kuweza  kutowa  huduma  ipasavyo .

Mgeni  rasmi  katika  hafla  hiyo  mbunge wa  jimbo  la bububu  mh  mwantakaje  haji  juma  amesisitiza  walimu  kujikubalisha   kuwa  ni walezi  kwa  wanafunzi  kwa kufuatilia  nyendo  zao  sambamba  na kuwapa  ushauri  ili  kuepukana  na  vishawishi  vitavyochochea  kuachana  na  masomo  katika  umri mdogo.

Kwa  upande wao  walimu  waliostaafu  wameahidi  kuendelea  kutoa  ushirikiano katika  kada hiyo  sambamba na kuwataka kuacha  muhali  wakati wa kutoa  maamuzi dhidi  ya  makosa   yanayojitokeza kwa  wanafunzi.