MPANGO WA KUDHIBITI MIMBA KATIKA UMRI MDOGO

 

Serikali ya mapinduzi ya zanzibar imesema imeandaa mpango wa kudhibiti mimba katika umri mdogo kwa wasichana ili kupunguza watoto wasiopata malezi ya wazazi wawili.

Akijibu maswali ya wajumbe wa baraza la wawakilishi, naibu waziri wa kazi uwezeshaji wazee vijana wanawake  na watoto shadya mohamed amesema mpango huo kwa asilimia kubwa utaondosha kero ya wasichana kupata mimba ovyo, hivyo wizara inajitahidi kutoa elimu katika maeneo mbalimbali juu ya madhara ya kupata mimba kabla ya ndoa.

Amesema mpango huo utaambatana na ule wa kupambana na vitendo vya udhalilshaji ambavyo vinazidi kushamiri kwa baaadhi ya watu kuendelea na vitendo hivyo.

Wakati huo huo waziri wa ardhi maji nishati na mazingira salama aboud talib ametoa ufafanuzi wa kupatikana nishati ya mafuta katika vituo vya mafuta hapa zanzibar.