MPANGO WA UDHIBITI KESI MAHAKAMANI UTASAIDIA KUSIKILIZWA NA KUMALIZIKA KESI KWA HARAKA

Jaji mkuu wa zanzibar mhe, omar othman makungu amesema mpango wa udhibiti wa kesi mahakamani kutasaidia kusikilizwa na kumalizika kesi kwa haraka mahakamani na kuongeza ufanisi wa kazi.
Mhe, jaji mkuu amesema mpango huo utaondosha kero kwa wananchi na majaji na mahakimu watafanya kazi zao kwa kufahamu muda wa kuanza kwa kesi na muda wa kumalizika kwa mashauri mahakamani.
Mhe makungu amesema hayo katika ukumbi wa mikutano tausi palace hotel kwenye mafunzo ya mpango wa udhibiti wa kesi mahakamani uliowashirikisha majaji, mahakimu na wadau wa mahakama.
Amesema mpango huo ukikamilika kesi zitakuwa na muda hadi kutolewa hukumu jambo litakalowezesha kuchukuliwa hatua kwa majaji na mahakimu wasiowajibika na kutaondosha kesi kukaa muda mrefu mahakamani.
Muwezeshaji wa mafunzo hayo dr. Zakayo lukumay amesema kwa sasa atakuwa na mamlaka ya kuwawekea muda majaji na mahakimu na kumaliza kesi jambo ambalo halikuwepo na kutoa mwanya wa watendaji hao kujiamulia muda wao wenyewe.
Mhe, khamis ramadhan ni naibu mraji wa mahakama kuu amesema waraka huo ukikamilika utaongeza kasi ya uchumi kutokana na wananchi watafahamu utaratibu mzima wa kesi zao mahakamani na kuondosha kero la kufatilia bila ya kujua muda wa kumalizika kwa mashauri yao.
Mhe ramadhan amesema awali kesi kazikuwa na muda wa kusikilizwa na kesi nyingi zilifika zaidi ya miaka miwili.