MPANGO WA UJENZI WA BARABARA ZITAZOHIMILI ATHARI ZA MVUA.

 

Wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji imesema haijapuuza kuzifanyia matengezo ya barabara ziliyoharibika na mvua za hivi karibuni ila inaendelea kufanya tahmini kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo makubwa.

Waziri wa wizara hiyo balozi ali karume amesema   tathimni hiyo inalenga kutayarisha mpango wa ujenzi  unaoweza kuhimili athari za mvua za masika katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza wakati akikagua namna barabara ya panga ilivyo athrika na mvua za masika waziri karume  amefahamisha kuwa kinachoendelea hivi sasa ni  ujenzi wa maeneo barabara muhimu ili kurahisisha wananchi kutumia miundombinu hiyo katika shughuli zao za maisha.

Mwakilishi wa jimbo la bumbwini mh mtumwa peya yussuf amesema  kuwa tangu kuharibika kwa njia hiyo wananchi wamekuwa wanausumbufu mkubwa huku wananchi wenyewe wakitoa ushuhuda wao.