MSITU WA JOZANI UPO KATIKA HATARI YA KUPOTEZA UMAARUFU WAKE

 

Mtafiti wa misitu kutoka nchini japan, amesema msitu wa jozani upo katika hatari ya kupoteza umaarufu wake endapo hakutakuwa na jitihada za uhifadhi kwa kudhibiti ukataji wa miti ndani ya  msitu huo.

Akiongozana na watendaji wa idara ya misitu na maliasili na maliasili zisizorejesheka, watendadi wa mamlaka ya vitega uchumi na wanajamii wanaopakana na msitu wa jozani, mtafiti huyo kentan neola, anaechukua shahada ya udaktari nchini japan, amesema watu wanahitaji kubadilika na kuona kuwa rasilimali zilizomo ni kwa ajili ya maslahi ya wote.

Ameongeza kuwa uharibifu wa msitu huo utapunguza kasi ya watalii ambao wamekuwa wakichangia mapato kwa wananchi na taifa kwa jumla.

Nd. Mzee khamis mohamed ni afisa uhifadhi, hifadhi ya taifa jozani, anaelezea aina ya miti na maisha ya baadhi ya viumbe wanaopatikana katika msitu huo.