MTAMBO WA KISASA WA X-RAY UTAKAOTUMIKA KATIKA KUFANYA UCHUNGUZI WA SAMPULI ZA MADINI

Serikali kupitia wakala wa maabara ya mkemia mkuu wa serikali imenunua mtambo wa kisasa wa x-ray utakaotumika katika kufanya uchunguzi wa sampuli za madini na kuwezesha kuboresha huduma za uchunguzi wa kimaabara.
Akizungumza na waandishi wa habari mkemia mkuu wa serikali pfofesa samweli manyele amesema mtambo huo uanojulikana kifupi kama edxrf umenunuliwa kwa dola za kimarekani usd 46,266 sawa na pesa za kitanzania shilingi milioni mia moja na moja, mia saba themanini na tano elf na mia mbili.
Amesema umesimikwa katika maabara ya mkemia mkuu wa serikali, kanda ya nyanda za juu kusini, mbeya ambapo mtambo huo utakuwa suluhisho kwa wizara idara na taassisi zake, wachimbaji wakubwa na wadogo wa dhahabu na madini ambao walihitaji kujua ubora na usalama wa bidhaa mbalimbali.
Profesa manyele amesema pia mtambo huo utatumika bidhaa za mbao ili kubaini kiwango cha kemikali zilizoko katika madini zinazotumika kutibu mbao na magogogo na kutengenezea bidhaa, pamoja na kupima sampuli za mafuta ya kupikia chakula, dawa, vipodozi, vipodozi na malighafi zake .