MTI WAUA WATU 20 MAPOROMOKO YA MAJI YA KINTAMPO, GHANA

Watu 20 wamefariki dunia na wengine wengi kujeruhiwa baada ya mti mkubwa kuwaangukia wakiogelea katika maporomoko ya maji eneo la kintampo, ghana.
Msemaji wa taifa wa huduma za dharura prince billy anaglate amesema kisa hicho kilitokea katika maporomoko ya kintampo, katika jimbo la brong-ahafo.
Bw anaglate ameiambia afp kwuwa watu 18 walifariki papo hapo na wengine wawili wamefariki wakiwa wanapatiwa matibabu.