MTIHANI WA KIDATO CHA NNE NA MAARIFA (QT) KUFANYIKA NOVEMBA 5 HADI NOVEMBA 23 MWAKA HUU

Baraza la mitihani tanzania (necta) limetangaza kufanyika kwa mtihani wa kidato cha nne na maarifa (qt) huku ikizitaka kamati za mitihani za mikoa, halmashauri na manispaa nchini kuhakikisha taratibu zote za uendeshaji wa mitihani hiyo zinazingatiwa ipasavyo.

 Mtihani wa kumaliza kidato cha nne ni muhimu kwani hupima uwezo na uelewa wa mwanafunzi kwa yale aliyojifunza kwa kipindi cha miaka minne ambapo matokeo yake hutumika kujiunga na elimu ya juu na wengine fani mbalimbli za utaalam wa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini dar es salaam katibu mtendaji wa baraza la mitihani tanzania (necta) dkt charlkes msonde amesema mitihani hiyo itaanza kesho novemba 5 hadi novemba 23 mwaka huu katiti shule za sekondari 4,873 na vituo vya watahiniwa wa kujitegemea 1,072 tanzania bara na visiwani.

Aidha Dkt Msonde amesema maandalizi ya mtihani huo yamekamilika ikiwemo kusambaza kwa mitihani, vijitabu vya kujibia na nyaraka zote kwa tanzania bara na visiwani.

Jumla ya watahiniwa 427,181 wamesajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha nne 2018 ambapo kati yao wa shule ni 368,227 na 58,954 wakujitegemea.