MTOTO WA GADDAFI AACHILIWA HURU

Mtoto wa pili wa wa aliyekuwa kiongozi wa libya muammar gaddafi ameachiliwa huru baada ya kuzuiliwa kwa kipindi cha miaka sita
Saif al-islam gaddafi, alikuwa anashikiliwa katika gereza la mji wa magharibi wa nchi hiyo ya kaskazini mwa afrika, zintan ameachiliwa chini ya msamaha wa wafungwa uilotolewa na bunge lililochaguliwa.
Mwaka wa 2015, mahakama ya libya katika mji mkuu tripoli ilimuhukumu saif al-islam adhabu ya kifo kwa mashitaka ya mauaji wakati wa vuguvugu la mapinduzi ya mwaka wa 2011 nchini humo ambae pia alituhumiwa na mahakama ya kimataifa ya jinai – icc kwa uhalifu wa kibinaadamu.